Dataset Viewer
Auto-converted to Parquet Duplicate
content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
SERIKALI imesema haitakuwa tayari kuona amani na utulivu wa nchi inachezewa huku ikisisitiza uwepo wa umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni wakati akifungua semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Da...
kitaifa
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesitisha likizo za viongozi wote mkoani humo kutekeleza maazimio ya Jukwaa la Fursa za Biashara la mkoa huo.Mwanri ameagiza kuwa, hata kama kuna likizo zimeidhinishwa zifutwe.Amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Msalika Makungu kuandika barua kwa viongozi kuhusu uamuzi huo na a...
uchumi
SERIKALI imetoa miezi sita kwa taasisi zote za umma ambazo hazitumii mfumo wa GePG katika ukusanyaji wa fedha kufanya hivyo na baada ya hapo itafanya ukaguzi na kuwawajibisha maofi sa masuhuli walioshindwa kutekeleza hilo.Akifungua mkutano wa mwaka wa kwanza wa watumiaji wa mfumo huo jana jijini hapa, Naibu Katibu Mku...
kitaifa
KAMPUNI ya mchezo wa kubahatisha ya M-bet imeingia makubaliano ya udhamini na timu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa miaka mitano wenye thamani ya sh Bilioni 1.Akizungumzia udhamini huo jana baada ya kusaini mkataba huo, Meneja Masoko wa Mbet, Allen Mushi alisema sababu ya kuiunga mkono timu hiyo ni baada ya ...
michezo
WATANZANIA wamekumbushwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa kuenzi amani, umoja na kulinda tamaduni za nchi ili kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza, ikiwemo vitendo vya ushoga na matumizi ya dawa za kulevya.Akizungumza wakati wa kutoa heri ya sikukuu hiyo ya Kuzaliwa Yesu Kristo, Kiongozi wa Waislamu w...
kitaifa
Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omary Kopa amesema wasanii nchini hawana umoja, na kwamba, wale wa bongo fleva na watu wengine, wanawaona wa taarabu ni watu wa hali ya chini na masikini.Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, kutokana na mtazamo huo, wasanii wa fani nyingine wamekuwa hawawashirikishi katika mam...
michezo
Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo aliyasema hayo jana ikiwa ni siku chache baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya mikopo ya viwanja jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyo atoke Dar es Salaam au Kibaha.Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ...
uchumi
IDADI ya vifo vya waendesha bodaboda nchini vitokanavyo na ajali imepungua katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu kinachoanzia Januari hadi Machi, ikilinganishwa na idadi ya vifo vya bodaboda kwa kipindi kama hicho kwa mwaka jana. Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Afande Deusi Sokoni akizungumza na...
kitaifa
Katika uzinduzi huo, rais amesema kuna haja ya kutafuta majawabu kuhusu namna ya kuongeza maghala ya kuhifadhia mazao kwani kadiri kilimo kinavyoboreshwa mazao yanayozalishwa yanakosa pa kuhifadhiwa.Rais Kikwete aliyasema hayo- Dar es Salaam juzi wakati akizindua kampuni hiyo ambayo itakuwa chini ya Mamlaka ya Soko la...
uchumi
KWA mujibu wa vyanzo mbalimbali, Tanzania ina makabila zaidi ya 120, yanayopatikana katika mikoa yote ambayo ndani yake kuna makabila zaidi ya moja. Makala haya leo yataangazia Kabila la Wabende linalopatikana katika Mkoa wa Katavi.Uchunguzi wa makala haya kupitia vyanzo mbalimbali umebaini kuwa, baadhi ya makabila me...
kitaifa
MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd amevihimiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini kurejesha ubora wao wa zamani kwa kuhakikisha wanaongoza kufanya vizuri katika michezo ya kitaifa na kimataifa.Kiongozi huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa mashindano ya Bara...
michezo
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewataka wateja waliokuwa na amana zao katika benki iliyositisha huduma zake ya FBME kuwa na subira, huku taratibu za kulipwa fedha zao zikiendelea.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Ha...
uchumi
MSEMAJI wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abbas amesema waandishi wa habari wanahaki ya kuikosoa serikali lakini hawapaswi kuandika habari za kuzusha na kupotosha.Amesema Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kifungu cha 32 (2) kinatoa haki hiyo ya kila mwandishi kuikosoa serikali na k...
kitaifa
Hayo yalisemwa na Rais wa TCCIA, Peter Chisawilo, hivi karibuni mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe kufungua mkutano mkuu wa mwaka na wa uchaguzi wa chama hicho mkoa wa Morogoro.Chisawilo alisema pamoja na kuunga mkono hatua ya serikali ya awamu ya tano kuhusu kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda...
uchumi
Rais John Magufuli amemteua Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo anachukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.Taarifa ya Ikulu iliyosambazwa mapema leo Jumamosi (Juni 8, 2019) imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Edwin Mhede k...
kitaifa
JESHI la Polisi linamshikilia mkazi wa Madale Mivumoni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ernest Alias (19) kwa tuhuma za kushiriki katika mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Mgaya(21).Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alibainisha hayo wakati akizungum...
kitaifa
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Joseph Iha, alisema huduma hiyo imezinduliwa wakati muafaka kipindi ambacho wateja wa benki hiyo wanazidi kuongezeka tangu kufunguliwa kwa benki hiyo hapa nchini.Alisema kwa kuzingatia ubora katika utoaji wa huduma, uo...
uchumi
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka washiriki wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili mambo ya nyuklia, kuhakikisha usalama wa watu, mazingira na mfumo wa ikolojia yanazingatiwa katika eneo la SADC kwa mujibu wa sheria.Alitoa mwito huo jana jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa wa...
kitaifa
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa NBS, Ephraimu Kwesigabo, alisema jana kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Juni imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwezi Mei.Hata hivyo, Kwesigabo alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi ...
uchumi
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ameanza operesheni maalumu ya kuzibana Taasisi ambazo ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Dara es Salaam kwa kutembelea ofisi moja hadi nyingine ili zilipe madeni yao katika muda uliopangwa.Katika ziara hiyo taasisi sita kati ya...
kitaifa
KOCHA wa Nigeria, Gernot Rohr ameibuka na kusema kuwa hapingi mfumo wa teknolojia ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) baada ya timu yake kushinda mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kuisni juzi katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).Mfumo wa VAR, ambao umeanza kutumika katika hatua ya robo fainali ya Afcon 20...
michezo
Akizungumza kwenye uzinduzi wa vilainishi hivyo vya magari jana katika kituo kipya cha mafuta ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo nchini, Phillipe Corsaletti alisema promosheni hiyo itafanyika kwa wiki kadhaa.“Castrol inaongoza duniani katika ubora wa utengenezaji, usambazaji, matangazo ya v...
uchumi
['Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale anakaribia kuondoka katika klabu hiyo kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Zinedine Zidane. ', 'Mchezaji huyo wa taifa la Wales aliwachwa nje wakati Real Madrid ilipolazwa 3-1 na Bayern Munich nchini Marekani.', 'Akizungumza baada ya mechi hiyo, Zidane alisema: Tunatumai ataondo...
michezo
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imetaifi sha mali zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 93.16 sawa na Dola za Marekani milioni 41 zilizotokana na uhalifu.Mali zilizotaifishwa ni madini, nyumba, magari, fedha za upatu, mbao na maliasili kwa kipindi cha mwaka 2013 hadi 2019 zilizotokana na uhalifu wa...
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema serikali ipo mbioni kuweka utaratibu utakaowalazimisha waingizaji na wazalishaji wa chupa za plastiki kuziondoa kwenye soko kunusuru mazingira.Makamba ameyasema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha Paper Craft International...
kitaifa
WABUNGE wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kurudisha zana za wavuvi zilizochukuliwa na kukamatwa wakati wa Operesheni Nzagamba II na wale walioziingiza nchini nyavu zenye saizi hizo ndogo wachukuliwe hatua.Wakichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa na Waziri Luhaga Mpina, wabunge wamesema nyavu z...
kitaifa
POLISI wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa inamshikilia William Sokoni (33) akidaiwa kumtukana matusi ya nguoni, mama yake mzazi, Clemensia Wangabo (77) na kumsababishia umauti.Mwanaume huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtenga inadaiwa alighadhabika baada ya mama yake mzazi kumtaka amlipe kiasi cha Sh 50,000 alizomko...
kitaifa
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafi sadi imemhukumu raia wa Nigeria, Christian Ugbechi (28) kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafi risha pipi 56 za dawa za kulevya aina ya heroin hydrochloride.Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji Sirri...
kitaifa
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inaridhishwa na misaada inayotolewa na taasisi za fedha za kimataifa, ikiwemo Benki ya Dunia.Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia uliofanya ukaguzi wa miradi ya Mfumo wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kwa upande ...
kitaifa
Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Woiso Original Products, Leornad Mtei, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.Alisema baadhi ya wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ya utengezaji wa ngozi, wamekuwa wakishindwa kutengeza bidhaa zenye ubora zaidi ya bidhaa zinazotoka nje, kutoka...
uchumi
Yanga ilimtambulisha mshambuliaji Ibrahim Ajib iliyemsajili kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika. Singida United imemsajili mshambuliaji Pastory Athanas aliyedumu miezi sita tangu ajiunge kutoka Stand United Shinyanga.Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga Jangwani na alikabidhiwa jezi namba 10 ...
michezo
WATU watano wakiwa ndugu wa kiume wa familia moja waliopigwa risasi na askari wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na kulazwa kwa matibabu katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Katavi, wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu ya kibingwa, ikiwamo kuwatoa risasi kwenye miili yao.Wanaume hao ni wakazi w...
kitaifa
KAMPUNI ya ndege Tanzania (ATCL) imesema haijaajiri wazee kutoa huduma kwenye ndege na pia wote wanaofana kazi hiyo wana sifa za kitaaluma kwa kuwa utaratibu wa kuwapata, umezingatia matakwa ya kimataifa yanayohusiana na kazi hiyo na si urembo wao.Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema jijini Dar es Sa...
uchumi
Serikali ya Kenya imetangaza kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa ndani katika miji mikubwa kufi kia Shilingi za Kenya 13,500, ambayo ni sawa na zaidi ya 300,000 za Tanzania .Lakini, kwa upande wake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema katika kuhakikisha mishahara inapanda katika sekta za um...
kimataifa
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeongeza udhibiti biashara haramu ya nyara za serikali, pembe za ndovu, madini, dawa za kulevya na vitu vinavyopita viwanja vya ndege.Hatua hiyo ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Hamad Masauni alipofanya ziara ya kukagua hali ya usalama katika Uwanja wa Ndege wa K...
kitaifa
KOCHA Mkuu wa Simba, Patric Aussems amedai kutoridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo Simba walishinda kwa mabao 2-1.Simba ilitwaa taji hilo ikiwa ni mara yake ya nne, wakati wapinzani wao Yanga wakilitwaa mara tano tangu kuanzishwa kwa mashin...
michezo
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman ameitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kurekebisha sheria zilizopitwa na wakati ambazo baadhi hazifanyi kazi tena.Suleiman alisema hayo wakati akiagana na wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Mazizini kutokana na ...
kitaifa
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limebuni mkakati maalumu utakaotoa fedha kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu, watakaoibuka washindi kwa kuandika mapendekezo bora ya kibiashara yanayohusu utalii, kilimo, nishati mbadala na masuala ya mazingira.Mkakati huo wa NEEC wanaoshirikiana na Ubalozi wa Uhola...
uchumi
FAMILIA ya Naomi Marijani, mwanamke anayedaiwa kuuawa na mumewe Khamis Luongo kisha kuchomwa moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, imesema bado haina imani kama ndugu yao huyo kuteketezwa kwa moto wa mkaa.Kauli yao hiyo imekuja baada ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kigamboni, Thobias W...
kitaifa
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) inatarajia kuendesha kampeni maalumu ya mfano, kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika eneo la mpaka wa Namanga unaoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.Kampeni hiyo inatarajiwa kuwa na matokeo chanya na kujenga uwezo wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko hasa kwa nchi hizo mbili.Taarif...
kitaifa
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amewataka baadhi ya wanasiasa nchini wanaobeza majadiliano yaliyofanywa baina ya Rais John Magufuli na viongozi wa madhehebu ya dini Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni kutubu kwa kitendo hicho.Aidha, amewaonya wanasiasa nchini kuacha ku...
kitaifa
BODI ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali imetakiwa kuhakikisha miradi inayotekelezwa na mashirika hayo inazingatia mipango na vipaumbele vya serikali na wananchi katika eneo husika.Hayo yameleezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati wa kufunga maf...
kitaifa
SIMBA tayari imemaliza kazi moja na inatarajia kuanza nyingine mpya kabisa. Ndiyo, wamemaliza vyema safari ya kupambana na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika! Simba imeingia hatua hiyo baada ya kucheza mechi nne za kimataifa na sasa inatembea kifua mbele ikitamba kila kona, si wachezaji wala viongozi....
michezo
Kwa matokeo hayo, Yanga imerejea katika nafasi ya pili na kuendelea kumfukuza mnyama kimya kimya kwa kufikisha pointi 43 ikizidiwa pointi tatu na Simba huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara 20. Jadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilikuwa suluhu na kuwafanya mashabiki wa Yanga kuwa na hofu wakihofia t...
michezo
Timu za taifa za Para Taekwondo na Taekwondo zilizoondoka nchini mwishoni mwa wiki na kwenda Morocco kwa ajili ya mashindano hayo ya Afrika ya Taekwondo.Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Machi 28-30 wakati yale ya Para Taekwondo, ambayo ni maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu, itaanza siku moja baadaye.Rwanda amb...
michezo
.Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa licha ya idara ya mahakama nchini kuendelea kufanya kazi nzuri bado inakabiliwa na upungufu wa watumishi.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ikiwa ni mwanzo wa kuanza kwa shughuli za mahakama, Jaji Mkuu ames...
kitaifa
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mohamed Said Dimwa wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliokuwa wakijadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016.Alisema ni kweli soko la mwani limekuwa likiyumba ambapo wafanyabiashara wa ndani wananunua kwa ...
uchumi
MWANAFUNZI bora matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, Hope Mwaibanje (18) wa Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Arusha, amesema anataka kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu.Kwenye matokeo hayo, Mwaibanje ameibuka kuwa mwanafunzi bora akiwa ana alama za 1.7 ikimaanisha kuwa amepata alama ya A kwenye masomo yake yo...
kitaifa
BAADA ya Mbwana Samatta (pichani) kuangushiwa lawama na mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kuwa hajitumi anapokuwa na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, hatimaye mwenyewe amefunguka kuhusiana na tuhuma hizo.Awali, kulikuwa na maneno ya chini chini kuwa Samatta ambaye ni nahodha wa Stars kuwa hajitumi anapokuwa ...
michezo
Akihutubia Jumuiya ya Sekta Binafsi nchini Kenya juzi, mkuu huyo wa IMF alisema hadhani kwamba EAC iko tayari kwa utekelezaji wa mpango huo na inahitaji kwanza kushughulikia masuala muhimu ndani ya nchi zao kabla ya kuunganisha fedha zao, kwa mujibu wa habari zilizorushwa na Radio Capital FM ya Kenya.Lagarde aliwasili...
uchumi
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara ,Yanga tayari wamewasili mkoani Shinyanga kuwafuata Stand United kwa ajili ya mchezo ujao utakaochezwa kesho. Jumla ya kikosi cha wachezaji 18 kikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Samwel Lukumay kilitua kwa ndege Mwanza jana, kisha kwenda Shinyanga kwa basi.Akizungumzia mchezo huo wa k...
kitaifa
BARAZA la Utendaji la Chama cha Mahakimu na Majaji Afrika Mashariki (EAMJA), litafanya kikao chake kuanzia leo hadi kesho kutwa, mwaka huu jijini Arusha.Katika kikao hicho, Mahakimu na Majaji watajadili Sera ya Jinsia ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuzalisha sheria ambazo zinawawezesha wanawake kupata haki mahakaman...
kitaifa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mshitakiwa wa pili, Alloycious Mandago anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni mbili pamoja na wenzake, kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).Mbali na Mandago, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfan...
kitaifa
['Ulikuwa uhamisho ambao ulimfanya Neymar kuondoka katika kivuli cha nyota wa Barcelona Lionel Messi. ', 'Hatahivyo raia huyo wa Brazil amegonga vichwa vya habari kwa sababu tofauti tangu alipojinasua kutoka katika mabingwa hao wa Uhispania na kuelekea PSG. ', 'Amefunga magoli 34 kati ya mechi 37 ili kuwasaidia kushin...
michezo
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku makamanda wa polisi wa mikoa nchini, kuyazuia mabasi yanayotoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa, kusafiri muda wa usiku kwa kisingizio cha kuhofia kuvamiwa na majambazi.Amesema hawana mamlaka ya kupanga ratiba ya mab...
kitaifa
WAVUVI wa soko la Msasani jijini Dar es Salaam, wameanza kunufaika na matokeo ya vita dhidi ya uvuvi haramu kwa kupata idadi kubwa ya samaki, hasa aina ya jodari.Gazeti hili limefuatilia undani wa suala hilo kwa siku mbili kwa kutembelea sokoni hapo na kukuta idadi kubwa ya wavuvi wakitokea baharini kuvua. Likiwa soko...
kitaifa
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema fedha za mfuko wa jimbo ni za wananchi wa jimbo la uchaguzi na sio za mwakilishi hivyo zinatakiwa kutumika ili kuleta maendeleo yao.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed ametoa msimamo huo wakati anajibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotaka wa...
kitaifa
TIMU ya Mwadui FC imefunguka kuwa wameshajikamilisha vilivyo kukabiliana na wapinzani wao Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 33 baada ya kushuka uwanjani mara 14, Mwadui wapo n...
michezo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, alisema mwishoni mwa wiki kuwa ni vizuri wafanyabiashara mkoani humo na Watanzania kwa ujumla wake, wakachangamkia fursa hizo na kuufanya mkoa huo eneo la kuvutia wawekezaji.“Dodoma ya leo siyo ya miaka ishirini iliyopita, kwani ina mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii pia n...
uchumi
NCHI wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinafi kiria kugeukia kilimo cha mianzi kama moja ya vyanzo vya fedha za kigeni kutokana na soko la bidhaa hiyo kuongezeka kwa kasi duniani.Kwa sasa, bidhaa zitokanazo na mianzi zinatajwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 7 (zaidi ya Sh trilioni 15.4 za T...
kitaifa
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Martin Ngoga amesema, Bunge hilo ni taasisi inayotafakari na kuchukua hatua muafaka kwa mujibu wa matakwa ya nchi sita wanachama wa jumuiya kutekeleza majukumu iliyojipangia.Ngoga ameyasema hayo alipozungumza na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi ya Bar...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi ameahidi kutoa raha katika tamasha la Simba linalotarajiwa kufanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba hufanya tamasha lao Agosti 8 ya kila mwaka ambapo hucheza hutambulisha jezi watakazotumia msimu mzima, wachezaji na mwisho hucheza mechi ya kirafiki na timu kut...
michezo
KAMPUNI ya Vodacom katika mwaka huu wa fedha ulioishia Machi 31, imefanikiwa kuongeza mapato yake ya huduma hadi kufikia Sh trilioni moja, sawa na ongezeko la asilimia 5.4.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi, ongezeko la mapato hayo limetokana na mapato kukua katika huduma za M-Pesa, huduma...
uchumi
KUTOKANA na mabadiliko ya wakati, kuongezeka kwa biashara ya silaha na matukio ya kigaidi duniani, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaunga mkono mabadiliko ya Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa kwa faida ya usalama wa nchi.Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela ...
kitaifa
“Tawi letu hili la kipekee litatumika kuhudumia wateja wetu wote wakubwa na kukidhi matakwa yao kikamilifu kwa kutoa huduma zote za kibenki za kipekee katika eneo maalumu. Jitihada hizi zinaenda pamoja na dhamira ya Benki ya Exim ya kutoa huduma bora kwa wateja wake katika nyanja zote,” alisisitiza.Manek alisema kuwa ...
uchumi
TANZANIA na Kenya zimekubaliana kuimarisha uhusiano ma ushirikiano hasa katika masuala ya kiuchumi, sambamba na kujenga uwiano wa kibiashara wenye maslahi ya pande zote mbili.Hayo yamebainishwa na Rais John Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta kufuatia mazungumzo ya faragha baina yao katika kijiji cha Mlimani kabla ya Rais...
uchumi
KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) inazindua safari ya kwanza kwenda Johanesburg, Afrika Kusini kesho. Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hatua hiyo ni mafanikio ya mpango mkakati wao ulioanza mwaka 2017, waliojiwekea kuhakikisha shirika hilo linapata mafanikio kwenye usafi...
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Waislamu nchini waendeleze utulivu, amani na uadilifu waliouonesha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kwa kufanya hivyo, watasaidia kukuza umoja wa kitaifa, uchumi na kuboresha huduma za jamii.Amesema ni vema Waislamu wakatambua uadilifu waliouonesha wakati wa mf...
kitaifa
KATIKA kuhakikisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inafanikisha vyema miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia bajeti, ilipunguza kutegemea fedha za nje kutoka Sh bilioni 775.8 ya mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Sh bilioni 547.38 ya mwaka wa fedha 2018/2019.Aidha serikali iliongeza fedha zak...
kitaifa
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani linalishikilia basi la kampuni ya Smart kwa kubeba nguo zinazodhaniwa kuwa hazijalipiwa ushuru.Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es ...
kitaifa
Yanga ilirejea Dar es Salaam Alhamisi, ikitokea Zanzibar baada ya kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi hatua ya nusu fainali dhidi ya URA kwa mikwaju wa penalti 5-4. Jumatano ijayo wanatarajiwa kucheza mchezo wa raundi ya 13 wa Ligi kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili, N...
michezo
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga ilitawala katika kipindi chote cha kwanza na ndipo ilipopata mabao hayo mawili. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 46 sawa na vinara Simba wanaoongoza kwa uwiano mzuri wa mabao wakiwa na mechi moja kibindoni. Simba sasa italazimika k...
michezo
WATU wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi, wameuawa na polisi wakati wakiwa kwenye majibizano ya risasi ndani ya msitu wa Kisanga Kijiji cha Kisanga Tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro huku wengine 19 wakishikiliwa.Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa alisema kuwa tukio hilo ni Mei 16 mwak...
kitaifa
RAIS John Magufuli amesema mgogoro wa ardhi wa vijiji 33 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kati ya wananchi na wawekezaji, utapatiwa ufumbuzi hivi karibuni, kwa kuwa ripoti ya Tume ya mawaziri wanane aliyoiunda, imeshakabidhiwa serikalini.Kauli hiyo ya Rais Magufuli ilikuja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mae...
kitaifa
Mkurugenzi wa Idara ya vyama vya ushiriki Daud Simba alisema hayo wakati alipozungumza na wanachama wa Elimu Saccos katika mkutano wa kufanya tathmini ya maendeleo ya Saccos hiyo.Simba alisema sheria nambari 4 ya vyama vya ushirika imeweka mikakati na malengo mazuri ya kuhakikisha vyama vya ushirika vinaleta tija kwa ...
uchumi
SHIRIKA la Kimataifa la Uhifadhi Viumbe Baharini na Wanyama (WWF Tanzania) wilayani Kilwa mkoani Lindi litatumia Sh 424,361,857.00 kwa ajili ya mradi wa kuboresha zao la pweza katika kijiji cha Songosongo, utakaokamilika muda wa miaka miwili.Mwakilishi wa Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Matrida Simfukwe alisema hay...
kitaifa
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) imepanga ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, FA ambapo timu kongwe za Simba na Yanga zitaanzia Dar es Salaam.Kwa mujibu wa ratiba hiyo ya raundi ya tatu itakayoshirikisha timu 64 iliyotolewa na shirikisho hilo Dar es Salaam jana, Simba itaanza na AFC ya Arusha na Yanga ...
michezo
['Mchezo wa kamari unaendelea kuenea barani Afrika haswa miongoni mwa mashabiki wa soka. Ni biashara sasa iliyo na thamani ya mabilioni ya dola kwa kampuni zinazoendesha biashara hii, lakini si vile kwa wanaocheza, amebaini mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi.', ' Alipotembelea Katika chumba kimoja katikati mwa jiji la N...
michezo
MIKAKATI ya uboreshaji wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) umezidi kushika kasi baada ya kukamilika kwa ripoti ya pili ya upembuzi yakinifu.China imesema iko tayari kutoa fedha za kuboresha reli hiyo na kinachosubiriwa sasa ni mchakato unaoendelea baina ya Tanzania na Zambia kuhusu namna bora ya kuiboresha reli hiy...
uchumi
TANZANIA imeweka rekodi ya dunia kwa ukusanyaji wa mapato, yatokanayo na sekta ya uchimbaji wa madini, hatua inayotokana na usimamizi mzuri wa rasilimali hiyo, ikichangiwa na mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na serikali katika sekta hiyo hivi karibuni.Hayo yalielezwa jana na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa ...
kitaifa
['Real madrid inajiandaa kumtoa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,30, kwa pauni milioni 70 kubadilishana na mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling ,24. (Sky Sports)', 'Chelsea wana mshambuliaji wa Crystal Palace na mchezaji wa timu ya taifa Ivory Coast Wilfred Zaha,26 huku mshambuliaji wa RB Leipzig Tino Werne...
michezo
MKAZI wa kijiji cha Mkwapa kata ya Namatutwe wilayani Masasi mkoani Mtwara, Sandali Omari (40) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili (jina linahifadhiwa) anayesoma Shule ya Msingi Mkwapa, baada ya kumdanganya kumpa kilo moja ya korosho.Akizungumza na gazeti hili...
kitaifa
End of preview. Expand in Data Studio

Dataset Card for Swahili News Classification Dataset

Dataset Summary

Swahili is spoken by 100-150 million people across East Africa. In Tanzania, for example, Swahili is one of two national languages (the other is English) and is the official language of instruction in all schools. News in Swahili is an integral part of Tanzania's media sphere. News contributes to education, technology, and a country's economic growth, and news in local languages plays an important cultural role in many African countries. In the modern age, however, African languages in news and other spheres are at risk of being lost as English becomes the dominant language in online spaces. The Swahili news dataset was created to bridge the gap in utilizing the Swahili language to create NLP technologies. It aims to empower AI practitioners in Tanzania and across Africa, making them integral in the preservation and utilization of the Swahili language. This dataset, sourced from various websites providing news in Swahili, is a powerful resource for NLP research and development, and your role in utilizing it is crucial. Curated explicitly for text classification tasks, the dataset categorises news content into six distinct topics, enabling the creation of robust NLP models that can more effectively understand and process Swahili text. Additionally, this dataset is included in the MTEB to evaluate the capability of embedders to classify Swahili news accurately. The high accuracy of this dataset is attributed to the human annotation process involved in its creation.

Supported Tasks and Leaderboards

  • text-classification: The dataset supports text classification tasks, particularly news categorization.

Languages

The dataset is in Swahili.

Dataset Structure

Data Instances

An example of a data instance:

{
  "content": "SERIKALI imesema haitakuwa tayari kuona amani na utulivu wa nchi inachezewa huku ikisisitiza uwepo wa umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni wakati akifungua semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha viongozi wa taasisi za Kiislamu, lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao.Naibu Waziri amesema mwelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi na nchi kwa ujumla.“Serikali hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote,” amesema Masauni.Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Alhad Mussa Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo kwa mifarakano kati ya taasisi mbalimbali kama ilivyokuwepo awali huku akisisitiza kuendelea kwa umoja huo ili jamii ipate kuendelea.“Sisi kama Bakwata tunaihakikishia serikali uwepo wa umoja na ushirikiano baina ya baraza na taasisi zingine na tofauti zetu hazipelekei kukoseana au kuvunjiana heshima kwahiyo tunaomba serikali iamini uwepo wa maelewano mazuri tu kwa maendeleo ya nchi hii,” amesema Shehe Alhad.Semina hiyo ya siku mbili imejumuisha viongozi wa taasisi 100 huku mada ya Nafasi ya Taasisi za Kiislamu katika Kuleta Umoja na Kuishi kwa Amani itajadiliwa.",
  "category": "kitaifa",
}
Downloads last month
122